Tuesday, September 20, 2022

Huduma ya Ku-design Lebo za Bidhaa

Lebo za bidhaa zinatengenezwa ili kuongeza taarifa au maelezo muhimu kuhusu bidhaa. Ili bidhaa iaminike au kuuzika wateja wanataka wapate taarifa muhimu kuhusu bidhaa kama;jina la bidhaa, jinsi ya kuitumia, tahadhari za kiafya, mchanganyiko uliopo, bei, taarifa za mtengenezaji,nk. 

Bidhaa yenye taarifa hizi inaongeza thamani na imani kwenye soko.







Huduma ya ku-design 3D Book Covers

 Kava za vitabu ni picha za kidigitali za kitabu ambazo zinaonesha pande tatu za kitabu. Kava hizi zinaelezea kitabu kinahusu nini au mtu atapata nini akikisoma.Kava hizi ni muhimu zaidi kwa wanaouza vitabu mtandaoni kwa sababu wasomaji hupima ubora wa kitabu kwa kuangalia kwanza kava lake.

Tunatoa huduma hii ili kuhakikisha kuwa wateja wetu wanapata kava nzuri,ya kuvutia na inayouzika.

Huduma ya Ku-design Birthday Covers

Kumbukizi ya siku ya kuzaliwa ni tukio muhimu kwani hutokea mara moja tu kwa kila mtu katika mwaka husika. Kutokana na ukweli huu siku hii inakuwa ni siku maalumu inayohitaji vitu vyake vya kipekee ili iwe tofauti za siku nyingine. 

Sisi kama POLAQUE DESIGNS tunatengeneza kava za siku ya kuzaliwa ili kuongeza thamani ya siku yenyewe.


Huduma ya Ku-design Business Cards

Hizi ni kadi ambazo zinabeba taarifa muhimu za kibiashara kama; jina la mhusika,jina la kampuni,cheo chake, Mawasiliano yake na mahali alipo au ilipo kampuni. Kuwa na kadi hizi inakuongezea thamani wewe kama mfanyabiashara.


Huduma ya Kudesign Mabango (Banners)


Mabango yanatumika kuonyesha/kuelezea biashara au huduma unayotoa hasa katika eneo lako la kazi.Bango pia linaweza kuwekwa sehemu yenye mkusanyiko mkubwa wa watu kama njia ya kutangaza soko la biashara au huduma unayotoa. Mabango yanampa mfanyabiashara urahisi wa kuonekana na kujulikana.

Huduma ya Ku-design Vipeperushi Mtandao (Posters Design)

Kukua kwa teknolojia kumesababisha watu wengi kutumia mitandao na hivyo kuleta fursa kwa wafanyabiashara na watu wengine wanaotaka kufikisha ujumbe kwenye jamii kuwafikia watu wengi kirahisi kupitia kwenye mitandao.Kazi ya vipeperushi mtandao ni kulifikia kundi hili. 

Vipeperushi mtandao vinavyovutia vinakupa fursa wewe kama mteja wetu kuwa tofauti na wa kipekee na hivyo kuzingatiwa kwenye ulimwengu wa intaneti ambao una vitu na kelele nyingi.

Monday, September 19, 2022

Huduma ya Kutengeneza Wasifu wa Kampuni (Company Profile Designing)


 Wasifu wa kampuni unasaidia kufikisha taarifa muhimu za kampuni kwa wateja au wafadhili kwa njia rahisi zaidi. Pia ni namna nzuri ya kuiweka kampuni kitaalamu.

Huduma ya kutengeneza Nembo (Logo Designing)

 Nembo ndio msingi wa chapa yoyote kwani inatambulisha chapa hiyo na kueleza inachofanya. Nembo ndio kiwakilishi cha chapa.

Kama ilivyo kwenye nyumba, msingi imara hujenga nyumba imara. Chapa yenye nembo nzuri na inayovutia ni msingi imara wa kuifanya chapa hiyo kuwa yenye mafanikio makubwa.