POLAQUE DESIGNS Tunajihusisha na utoaji wa Huduma za Graphics Designing,Blog Designing na Digital Marketing.Tuna uzoefu wa Miaka miwili.
POLAQUE ni muunganiko wa maneno mawili; POLARIS na QUEZON. POLARIS ni nyota inayong'aa iliyopo katika anga la kaskazini (Northern Pole). Nyota hii hutumiwa na wasafiri wa majini kama dira ili kujua uelekeo kwa sababu ina sifa ya kutulia sehemu moja tu. QUEZON ni mji mzuri uliopo nchini Ufilipino.
Muunganiko wa maneno haya unaleta jina POLAQUE lenye maana ya " Dira imara kuelekea kwenye kitu bora/kizuri.
Maono:
Maono yetu ni kuwa chaguo nambari moja katika utoaji wa huduma zetu ukanda wa Afrika mashariki kwa kutoa huduma bora na kwa ubunifu mkubwa.
Dhamira:
Dhamira yetu ni kuwezesha upatikanaji wa huduma zetu za kimtandao kwa watu wa hali zote za kiuchumi na kusaidia wateja wetu kufikia malengo yao kupitia huduma tunazotoa.
Kauli Mbiu:
Tunakutengenezea njia kuelekea kutimiza ndoto yako.
No comments:
Post a Comment